Pages

Friday, December 23, 2005

NINGEKUWA NA MABAWA....

Ningekuwa na mabawa ningeruka upesii..Nyumbani mbali..ni nani asiyepata ugonjwa wa kukumbuka nyumbani hasa inapofika wakati wa sikukuu???????Ninatembea barabarani,ninatazama huku na kule nikijaribu kubadili mazingira kwa akili na macho yangu,nafunga macho, nafungua ni pale pale ambapo nimekuwepo,hakuna jipya zaidi ya mapambo na harakati za sikuuu..
Heka heka za manunuzi ya mwisho mwisho wa sikukuuu ya Noeli ndio hivyo yanatia tamati muda si mrefu.Ni maduka makubwa machache ambayo yatakuwa wazi.Watu wanasafiri,barabara ,viwanja vya ndege vimejaa watu wako mbioni kuungana na familia na mrafiki kwa ajili ya sikuuu.Hizi ni harakati ambazo zinaendelea kwa hali ya juu hapa nilipo.Wafanyao kazi,wengi wao wanasiku kadhaa za mapumziko.Ni shamra shamra zinaendelea hapa Nyumbani kwa Joji Kichaka.
Ninakumbuka nyumbani,ninakumbuka Tanzania,ninakumbuka Dar-es salaam,Ninakumbuka Rombo.Nauli za kuelekea Kilimanjaro zimekuwa "iyo la njofuu"Kila mtu anataka kupanda basi la Meridia kwenda Rombo.Watu wamekuwa wengi nauli haishikii..lakini hakuna anayekubali kusherehekea noeli darisalama.Maamuzi ya kukaa kwenye kigoda masaa nane yanawakumba wasafiri wa dakika za mwisho .Hiyo ndio hali halisi,kituo cha basi cha ubungo kimeshehena watu..ni majira ya saa tisa na nusu na kumi alfajiri mabasi yanaondoka.Yameanza kuwasha taa na honi zikipigwa kwa wingi.Ni mashamu shamu na manjonjo ya sikukuu tu hayo.Bila kusahau polisi wa usalama barabarani nao wanamengi ya kusema na madereva.
Ni foo shuruni kulwayaa mndeni,waiinu waliisha isherikia krismasi,mengele si meshiha,si isafii,umbe sa amii fo shii,mahorima.Kwentrwe maruwa,umbe silishinjwa,mburu,kisusio,umbeke kwentre kila mrii..ndisi na mshele umewa tayari kwa jumapili we kora pilau na shapati.Kwa fungua redioo waishua foo Kenya wakakaba Jim revees nyimbo saChirsmas.Foo makaniseni kwentrewe misa sa kiyoo,hashe hashe kona waliimba.Ngaamba kwentre chrismas mndeni laaya handu we manya kwetre skukuu.
HASHE HASHE KONA !!

Wednesday, December 14, 2005

Kumekucha.

Hivi siwezi kuaminini mwezi sasa umepita tangu niingie humu ndani ya nyumba yangu kusema lolote.Hivi ni mwaka huu umekuwa mfupi au nimekuwa na mambo mengi kIasi nasema kuwa muda ulikuwa mdogo.
kuna mwanablogu mmoja huwa anasema masaa 24 huwa haya mtoshi na sema tena sasa nimeamini nitaacha kutania ambao wanadai masaa 36.
Mchana wa leo umekuwa mtulivu kidogo kwangu baada ya kumaliza mitihani yangu ya muhula kama lisaa limoja lililopita.Nimerudi katika ulimwengu wa kutoa maoni yangu kwa kutumia mtandao.
Ulimwengu wa Blogu umekuwa na mafanikio bila kipingamizi na kuna mwamko wa pekee unaendelea katika jamii ya waafrika wazungumzao kiswahili.Na hao sio wengine ni wa Tanzania wenzangu ambao wamekuwa wakijiunga kila siku kukicha katika hii tekinolojia.Nasema tena karibuni watanzania wenzangu tuweke yanayotusibi hata kama hawasomi watayasikia kupita hapa ama pale.Hongera sana kwa wale ambao wamekuwa wakijiunga kwa wingi,naweza kusema mwaka 2005 umekuwa na changamoto ya pekee kwa wana globu.Hongera kwa watu ambao hawako nyuma kutupa viunganishi vya globu mpya mara zinapoingia..si Mwingine bali ni NDESANJO.http://jikombe.blogspot.com

Monday, November 14, 2005

Sema utakacho.

Mfiri n'ganyaa fo nyumaa nilikuwa natembelea blogu mbali mbali na kuangalia nini hasa kinaongelewa na nini hasa, nani anajisikia kuandika nini.
Nilifurahi sana na dhani nilitumia muda wa masaa mawili tu kusoma nini wanablogu kama mimi wanasema na kujifunza.
Siku kadhaa niliahidi nitaandika kuhusu televisheni.Laah leo nimepata zuri zaidi lipi hilo.
Nimeingia katika fani ya afya.Nilikuwa nasoma kuhusu mkojo na tiba zake.Ahh ni mengi nitaandika tena .Bado nasoma makala tofauti tofauti kupitia wandishi tofauti na kurasa tofauti za mtandao.

Monday, November 07, 2005

je huu ni ubaguzi??

Nina kazi ya darasani ya kuandika kuhusu jamii na utazamaji wa luninga.nimeshindwa kusema ama kuandika vizuri kutumia kiswahili hata kile kichaga.mada yenyewe inasema hivi"Ethinicity&race has been a long time issue on television."
Hapa nitakuwa nazungumziua jinsi televisheni zimekuwa zikionjesha aina fulani za jamii na yanayowazunguka.. katika vipindi vya luninga kama "friends"Bill Cosby"oprah na wengineo.Je wanaonyesha ule uhalisia wa jamii zao.?Je jamii ndogo kama za wamarekani halisi (wahindi wekundu)wamarekani wa kiasia?Je hawa wamekuwa waki wakilishwa katika hivi vipindi?Nitarejea nikimaliza kuandika kazi yangu ya shule.Hii mada imenikumbusha mengi.

Saturday, October 22, 2005

Ni kweli??

Ni imani tu au ni kweli??Hizi baadhi y aimani za watu ambozo nimekuwa nikiziskia masikioni mwangu..Na aliyenikumbusha haya ni mwana blogu mmoja aliyekuwa amepanga safari mambo yakataka kuharibika dakika za mwishohttp://jikombe.blogspot.com.
  1. Hii inatoka kule nyumbani kwangu...Rombo ...Ukiwa unasafiri usibebe ndizi za mzuzu...wala kuzila asubuhi yake safari yako itakuwa ina ..mikosi...wakimaanisha kuharibikiwa gari,kupoteza mzigo na mengi yajirijo katika safari hasa ikiwa safari ya masaa kadhaa.
  2. Si vizuri asubuhi ukakutana na mtu amevaa sweta,shati au nguo yoyote ya juu halafu amechomeka mikono ndani...kama vile watu wa vaa avyo kama unasikia baridi huku ukita kukunja mikono ndani.Chukua tahadhari na wewe fanya haraka ingiza mikono ndani uuepeku hicho kisirani.
  3. Kufagia nyumba usiku ....si vizuri
  4. Hii ni ya kimarekani...usimfagie mtu miguu...nikimaanisha ukiwa unafagia usilogwe ukamsogelea mtu na ufagio wako mbele ya miguu yake atakukimbia na kukuogopa..Hicho ni kisirani
  5. Usitumbee /kukatisha chini ya ngazi..Ngazi zile zinazotumika kuchukulia vitu juu(ladder)Hii ni hatari kabisa(Marekani)
  6. Kukaa kwenye kizingiti cha nyumba baada ya saa 12 jioni..na kama ulikuwa umelaa mchana, saa 12 jioni ikakukuta kitandani.Inasemekana unaweza kuamka unaumwa(Pwani...Tz.)

Hizi baadhi ya zile imani fulani fulani nilizozikumbuka!!

Monday, October 10, 2005

hivi ndivyo ilivyokuwa.

Safari ikaanza kuelekea huko ambako kimbunga kilikisiwa kutokufika.Safari ilianza kwa matumani huku kila mtu akiwa na matumaini ya kufika salama.Kasheshe na mauza uza uza yote yalikuwa barabarani.Ulikuwa ni msongamano wa magari ambao ulikuwa wa kwanza kwa mimi kuona kwa macho yangu.Na huu msongamano ulikuwa katika zile barabara za juu ambazo hutumika kwa mwendo kasi.magari hayasogei...hali ya hewa inazidi kuwa ya hatari.Huku kwenye redioni, meya wa jiji anazidi kuonya kuhusu umuhimu wa kuhama mji na maeneo ya hatari.
Nimekesha usiku kucha barabarani...hakuna matumaini yoyote yale sasa ni saa 12 asubuhi..sijaweza hata kutoka nje ya mji.Muda wa saa 24 nipo barabarani sijaweza hata kufika upande wa kaskazini wa mji ninaoishi.Imefika saa 1 asubuhi nasikiliza redio tunaelezwa kwamba barabara ya kuelekea kusini itafungwa iruhusu magari kuelekea kaskazini.Nimechoka nina usingizi ninahofu ya mvua kuanza nikiwa barabarani.Ninahofu ya kupoteza maisha ,majira ya joto hayaisha rasmi katika huu mji wa Houston joto ni kali mno, la nyuzi za farenihaiti 94.
Nimechoka sasa naona hakuna matumani ...ninafikiri jambo moja tu hapa nilipo nikaribu na nyumbani kwa rafiki yangu aishiye kaskazini.Ninakata shauri na kwenda kupumzika kwake...huu ni mchana wa siku ya alhamisi alasiri.Hali ya hewa bado ni mbaya upepo unaoleta hilo janga unazidi kuvuma.Mawasiliano ya simu yameshakuwa mabaya kutokana na kila mtu kuwa ni mtumiaji wa simu kwa wakati mmoja.Mafuta ya magari sasa yamekwisha katika vituo matumaini ya safari yanapungua.Ninakaza roho nina pumzisha mwili usiku wa alhamisi.
Ni Ijumaa siku ambayo mvu haribifu na kimbunga inaanza ifikapo saa 6 usiku.Ninadamka mapema nakuanza kuangalia televisheni napata matumani .Mafuta ya gari yanapatikana sasa ..serikali imeamua kusaidia wananchi mafuta.Hapa naona Jeuri ya Joji Kichaka...na fadhila zake .Ninafanya hima kuondoka kaskazini na kuanza upya safari.Safari sasa inaahueni...na matumani yapo .Inanichukua masaa 4 kufika katika mji wa Dallas.Imeshakuwa jioni sasa ni majira ya saa kumi..nina jinyoosha kidogo..Kuanza upya safari ya masaa 6 kuelekea kansas.
Safari inakuwa ni ndefu ila yenye matumani makubwa nimeweza kuondoka eneo la hatari.Ni saa sita usiku ninafika mji wa Kansas...ninatazama televisheni naona mvua imeshaanza kunyesha Houston na hali ya hewa ilivyotabiriwa inatoke.Ninajipatia mapumziko ya siku mbili hapa mndeni(mashambani) Kama vile wenyeji wauitavyo.
Siku ya Jumapili ninarudi nyumbani mambo yalikuwa shwari hakuna baya sana la uharibifu lililotokea.

Monday, October 03, 2005

SAFARI IMEIVA!

Siku,masaa, dakika na hata mwezi sasa unakaribia kuisha tangu ..Sekeseke za mvua za ughaibuni zijulikanazo kama hurricane zipite.Haya mambo yote yalianzia kule Luissiana ambako karibia kila mali iliteketea.,viwanda nyumba,shule ,hospital na sekta zote muhimu.
Basi shughuli na mihangaiko hayakuishia hapo basi sisi majirani wa Luissiana nasi tukapata joto ya jiwe ilikuwa ni kipindi kisicho zidi majuma manne.
Basi hizo hekaheka zikanifika hata mimi mbiu ikapigwa.. kila aliyeko eneo la hatari na hicho kimbembe basi aondeke.Na mimi nikawemo..Nayosema hapa yasikie tu yakikufika utajua.
Basi safari nikaanza siku ya Jumatano mnamo saa tano na nusu nikiwa na lengo la kuelekea Kansas mji wa mbali kutoka hapa nilipo.Muda wa makadirio wa kusafiri ikiwa masaa 6 barabarani.Haya basi hapa ndio nilijuinga na ule uhamaji mkubwa ambao unakaribia kuwekwa kwenye historia ya Marekani.
NITARUDI HIVI PUNDE KUENDELEA NA HIYO HABARI!

Monday, September 12, 2005

Yasikilizie kwenye bomba!!

Haya jamani kwa wana blog ambao walikuwa wanashangaa huyu mtu kapotelea wapi...???Basi ondoeni wasiwasi nilikumbwa na matatizo ya Rita..
Nasema tena haya mambo ya mvua za ughaibuni na upepo na vimbunga hivyo..Niliviona huku niliko.Almanusura maji yazidi unga .
Nina mengi ya kusema na kuandika ...Ndio kwanza huku mambo yamerudi kwenye mstari rasmi leo.

Thursday, September 08, 2005

Nimekubali

Hayawi hayawi sasa mambo yanazidi kuwa matamu katika ulimwengu wa kublog wa watanzani.
Yule mpiga picha maarufu na machachari wa Tanzania yupo ndani ya nyumba mtembelee tafadhali.www.michuzi.blogspot.com

Wednesday, September 07, 2005

Mnyonge Mnyongeni!!!

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni...unaweza ukakaa ukaona yanayotendeka hapa ulimwenguni ni kama ndoto za Alinacha kumbe ni kweli.
Ni juma hili ulimwengu umeshuhudi watu wakifa kwa mafuriko ya maji,njaa,kukosa msaada katika nchi ambayo inaheshimika duniani kwa ubabe.Na ni ubabe hasa wa kisiasa kiuchumi,kivita ikiacha watu wake wakigharaghara barabarani.Ni nchi hii hii ambayo inaendeleza ubabe kule mashariki ya mbali ikidai inawasaidia .Laa huku wakiwa na mambo na mipango yao mingi nyuma ya pazia.
Hali ya maisha ya hawa ndugu zetu,jamaa wa luisiana inasikitisha...Ilichukua serikali kufahamu ,maaafa ni makubwa baada ya juma.Mbona wao wanakuwa wababe hasa kwa watu wa nje kuliko kwa ndugu zao wa ndani.hapa mimi najiuliza au tunarudi kulekule kwamba Maskini ni maskini??Hata hivyo jamani kuokolewa siku za mwanzo haikuwa haki yake???Si hawa watu ambao wanapiga vita vifo visivyokuwa na misingi???Au tunarudi pale kwenye suala la rangi?
Nimekumbuka iliwachuikua muda kufikiri hilo kwa sababu ya wengi waliokuwa kule walikuwa ni weusi..na viongozi walio juu ni weupe.hivyo swala la kufikiria mtu mweusi lilikuwa mbali kiidogo.Inasikitisha kuona jinsi watoto wanavyopata shida wazee,wasiojiweza.
Ama hakika sasa Dunia imeona upande wa pili wa sarafu..Iliku ikishuhudia picha za watoto wa Sudani na nchi nyingine za kiafrika zikitaabika..Sasa wameona hata Marekani inaweza kuwaacha wananchi wake nao waonekane kwenye CNN .

Friday, September 02, 2005

petrilori

linu ngimemannya uishwa wa fitrwa fya Iraq..Mafutra yameituma ho dokaa yalishika dola itanu ha Marikani.Ngaammba Kishaka alefikiri iinda Arabuni mafutra yangesokaa yave sumni,laa mmeku yameinda hoo dokaa.Na mfua sa Lusiana.
Amba matukiooa yaika soni,mafutra,mfua,wanajeshi waliifa bure kulya irak.
Ngaamba pertilori ishingi nga foo Tz???

Wednesday, August 31, 2005

Ruwaaaa!!!!

Mfiri..majumaa yamiinda mwakaa ulutrumbuka..mweri wa nani umesia linu..

Ukakaa ukafikiri kiki uleruunda kwa mwakaa uu we si ng'ndo foo.
Ijumaa ili ngimemekubwa na mafkara soni kedekedu ..mamrasa aka alekubwa na mfua ilya ya fkorokoro mrii wose ukavaa mringa kwende barabara foo..kwende umeme foo kwentre chao..washeku ,wameku ,vana wamelia njaa,..vandu wamefaa..Kishaka ametruma ndumaa kwa kila mndru isadii...telefisheni si onyiosha kila saa..vandiu wasakwee.
Sumani ingia imeshaa haa..Imeikaa soni..Ilala uwanja wa mpira na wana ..kwennter ngo'ndo choose wetre..

Wednesday, July 20, 2005

Je utaanza lini!!

Hili jambo la kujali mazingira na kuheshimu kilichoachwa na kizazi kilichopita kimekuwa ni hadithi...na simulizi sizo isha katika masikio ya wanajamii...
Utunzaji wa mazingira huanzia na wewe mwenyewe kupenda kuvuta hewa safi na kujali kizazi kinachokuja.
Ni hivi karibuni nimekuwa nikisoma makala ya mazingira na kufahamu ubaya zaidi wa hizi hewa chafu ambazo binadamu tuna tengeneza.Tunatengeneza vifaa ambavyo tunatumia kwa muda usiopungua miaka kumi huku vikiachaa maafa ya miaka mia moja ijayo.
Kila siku inapokucha mwanadamu anawaza ni jinsi gani atarahisisha hiki bila kujali ni wa ngapi atakao waathiri.Gesi za magari na mashine nzito nzito ,bandari zinazoshusha mizigo huku zikipuliza gesi zinazochafua anga na kuhatarisha maisha ya viumbe hai,watoto,watu wazima na wazee.
Ni wakati sasa umefika wa kuanza kufikiri na kuweka mtazamo makini kuhusu mazingira.Maana kizazi kijacho kitakuja kutoa hukumu ambayo wewe na mimi tungeiepuka leo hii.
Tunza mazingira,achana na tabia ya kutumia mifuko ya nailoni,chupa za plastiki,kuendesha gari kwa umbali mfupi,tumia usafiri wa umma,acha kutumia madawa kumwagilia bustanini
Kwa wale wanaoweza leo hii amua kutumia gari linalotumia maji tu ama..mafuta ya mimea.Tunza mazingira na yatakutunza..

Thursday, June 23, 2005

Nimerudi!!!

Ngiletrondokia mfiri so siliso enda ...Ilikuwa ni katika harakati za kukimbizana na vitabu vya majira ya joto...Sikujua kuwa ingekuwa hivi...
Nimefurahi leo, narudi nakuandika...Joto limeshakuwa kali...foo njaa kwetre muu...irike...
Kwa wale waliodhani nimeingia mitini Nimerudi niko kamili....

Tuesday, June 07, 2005

KUWA MAMA!!

Haki kubwa kuliko yote duniani ya mwanamke ni kuwa mama .

Mwanzo ni mgumu!!

Nimekuja katika lugha mama...lugha ambayo nilijifunza kuongea kabla ya hizo zingine nizijuazo leo hii.Unapojifunza kuongea huwa unajifunza kwa ishara kwanza ndipo mambo mengine yana kuja.Ndio mwanzo wa kuanzaa kusema...maaa...ukimaanisha mama..pa..ukimanisha baba..
Je ulikuwa unajua kuwa watoto wadogo ambao wanajifunza kuongea ni vizuri ukawafundisha lugha ya Ishara kwanza?Inasemekana watoto wanaojifunza lugha ya ishara wanakuwa wepesi zaidi kuongea.
Je ulikuwa unajua kuwa kujifunza chombo cha muziki humsaidia mtoto katika ufahamu wakati wa ukuaji?Hata wewe pia unaweza kujifunza...hii haijali umri wala muda...Hakuna kitu kizuri kama kufanya kile upendacho katika muda uupendao?Hakuna kitu kizuri kama kufikia lengo lako......
"HAKUNA JAMBO GUMU CHINI YA JUA"

Friday, June 03, 2005

mfua na muu!!

Mfua na muu fyoose fyetre manufaa wakwe..ngaamba uleininga usaakwe kimu...wesakwaa muu ,mfuu??

Monday, May 30, 2005

kimo ksalele!!

Kwentere ng'ondo fyeni nimara eese..haa linu na ng'amaa kwentere mfua na fkorokoro..fo njaa..motro umekatika haa ...ukanikumbusa darslamu...
Ngili na mwana wakwa ...amelia lini kwa ajili ya fkaro koro..amelala motreka...nami ngaasa iandika ...uuhhh..ngiinde ilala..for ng'amaa see..

Tuesday, May 24, 2005

kimanye choose

kwentere muda ngafikiri na imanya kwentre ngi'ndo ksha sha imanya itrerta lugha sa kiune...imanya lugha so kwe kusaidia shule ,kasini ,na foose wenda...
Ngilimanya kishaka mfiri so silosiha ngieveandika ngisheko...amba ngiishi foo.Manya itengenesa matreta haa ingi urunda nusu mfiri iandika...Ngiliiinda shule kapisa kingimanye ....

Monday, May 23, 2005

kishaka kikiumu

Linu nimefikirii...ngaamba kishaka kikuumu itretra ..iaindika..,
Ngilimemanya foo...Ngile fikiri na kuitani ili ka swahili oo kiingeresa..
Ngisaidieeni washaka!! waoose..

Friday, May 20, 2005

Ummeku /msheku kuinda daresini

Kuinda shule or daresini kwetre umri ohh iseeka...mfiri silisosiha kwentre mndu aliiyee malisa shule entere miaka sabini na iwa daktari wa wanyama...Ngaamba wameku na washeku wa haa..weenda shule kila mfiri...ngilisoma shule na darasa lakwa letre msheku wamiaka keseee.
Ngaamba wameke,washeku indeni shule..iseeka kwentere ng'ondo foo...

Wednesday, May 18, 2005

Yaliyojiri!!

Basi katika kutafuta nini kinaendelea katika Tanzania au bongo wengi wasemavyo ...Nimekutana na habari ya kunifurahisha.."sasa Sumaye Raisi"Si utani nenda hapa www.darhotwire.com

Tuesday, May 17, 2005

ngimetirima...

Ngaamba see kishaka na findo fya kieni...ni ng'indo kimu..
Ngashukuru...womi na wose waliondika...Uwiii hasa msasha akwa Mkwenda..na Ndesanjo ...
Haya basi asante sana mlionipomgeza kazi inaanza rasmi...

Monday, May 16, 2005

HAYAWI HAYAWI .....YAMEKUA

Hivi ndivyo navyoaanza kwa kusema....hayawi hayawi yamekuwa...nimeingia rasmi katika ulimwengu wa kublogu...kazi kwenu..
Je unajua utakuwa unapata nini hapa??????? Mchanganyiko wa mawazo,maoni,utafiti na mengineyo katika lugha mbili tofauti..nikimaanisha kichagga na kiswahili..Mtu kwao!!!Jivunie ulichonacho ....kabla hakijaondoka .Na kwa kuanza kabisa tunaanza kufungua mawazoo na kuweka Ukweli mbele na kuondoa fikra za "hatuwezi,siwezi,"Na kufahamu wewe ni nani.
Ngaaamba see...ife ni nifi?

Thursday, May 12, 2005

Ngakuia kindo???

Ngakuia kindo kishaa linu??Foonjaaa kwentrwe muu ...umetirima kwa amba muu wa Talaha kwa
shekuyo....ngiliinda uusakwa ngimanyime kisha nkiiii ngilifinya...shule nilefunga hiyoo..
Mtwemeni ni nng'amaa ...

Wednesday, May 11, 2005

MLAAFO WOMI WA LONGONI NA WAFELE??????

Ngiliinda shule kapisaaa ngimanye kishaka...ngilijifunza kimu kimu haki...ngimanyee chooosee.
kimeksalele..ngilijifunsa ngiandike fitabu...shekuyo asome na voose..ngii jifunse iringi kapisa ngiwafuswe womi na wafele wakwa kona....wamwaii..wamanye kishaka cha Horombo na darslamu.....
KUMEKYA MACHA......NGILIJARIBU KITA KITAA.....