Pages

Saturday, October 22, 2005

Ni kweli??

Ni imani tu au ni kweli??Hizi baadhi y aimani za watu ambozo nimekuwa nikiziskia masikioni mwangu..Na aliyenikumbusha haya ni mwana blogu mmoja aliyekuwa amepanga safari mambo yakataka kuharibika dakika za mwishohttp://jikombe.blogspot.com.
  1. Hii inatoka kule nyumbani kwangu...Rombo ...Ukiwa unasafiri usibebe ndizi za mzuzu...wala kuzila asubuhi yake safari yako itakuwa ina ..mikosi...wakimaanisha kuharibikiwa gari,kupoteza mzigo na mengi yajirijo katika safari hasa ikiwa safari ya masaa kadhaa.
  2. Si vizuri asubuhi ukakutana na mtu amevaa sweta,shati au nguo yoyote ya juu halafu amechomeka mikono ndani...kama vile watu wa vaa avyo kama unasikia baridi huku ukita kukunja mikono ndani.Chukua tahadhari na wewe fanya haraka ingiza mikono ndani uuepeku hicho kisirani.
  3. Kufagia nyumba usiku ....si vizuri
  4. Hii ni ya kimarekani...usimfagie mtu miguu...nikimaanisha ukiwa unafagia usilogwe ukamsogelea mtu na ufagio wako mbele ya miguu yake atakukimbia na kukuogopa..Hicho ni kisirani
  5. Usitumbee /kukatisha chini ya ngazi..Ngazi zile zinazotumika kuchukulia vitu juu(ladder)Hii ni hatari kabisa(Marekani)
  6. Kukaa kwenye kizingiti cha nyumba baada ya saa 12 jioni..na kama ulikuwa umelaa mchana, saa 12 jioni ikakukuta kitandani.Inasemekana unaweza kuamka unaumwa(Pwani...Tz.)

Hizi baadhi ya zile imani fulani fulani nilizozikumbuka!!

Monday, October 10, 2005

hivi ndivyo ilivyokuwa.

Safari ikaanza kuelekea huko ambako kimbunga kilikisiwa kutokufika.Safari ilianza kwa matumani huku kila mtu akiwa na matumaini ya kufika salama.Kasheshe na mauza uza uza yote yalikuwa barabarani.Ulikuwa ni msongamano wa magari ambao ulikuwa wa kwanza kwa mimi kuona kwa macho yangu.Na huu msongamano ulikuwa katika zile barabara za juu ambazo hutumika kwa mwendo kasi.magari hayasogei...hali ya hewa inazidi kuwa ya hatari.Huku kwenye redioni, meya wa jiji anazidi kuonya kuhusu umuhimu wa kuhama mji na maeneo ya hatari.
Nimekesha usiku kucha barabarani...hakuna matumaini yoyote yale sasa ni saa 12 asubuhi..sijaweza hata kutoka nje ya mji.Muda wa saa 24 nipo barabarani sijaweza hata kufika upande wa kaskazini wa mji ninaoishi.Imefika saa 1 asubuhi nasikiliza redio tunaelezwa kwamba barabara ya kuelekea kusini itafungwa iruhusu magari kuelekea kaskazini.Nimechoka nina usingizi ninahofu ya mvua kuanza nikiwa barabarani.Ninahofu ya kupoteza maisha ,majira ya joto hayaisha rasmi katika huu mji wa Houston joto ni kali mno, la nyuzi za farenihaiti 94.
Nimechoka sasa naona hakuna matumani ...ninafikiri jambo moja tu hapa nilipo nikaribu na nyumbani kwa rafiki yangu aishiye kaskazini.Ninakata shauri na kwenda kupumzika kwake...huu ni mchana wa siku ya alhamisi alasiri.Hali ya hewa bado ni mbaya upepo unaoleta hilo janga unazidi kuvuma.Mawasiliano ya simu yameshakuwa mabaya kutokana na kila mtu kuwa ni mtumiaji wa simu kwa wakati mmoja.Mafuta ya magari sasa yamekwisha katika vituo matumaini ya safari yanapungua.Ninakaza roho nina pumzisha mwili usiku wa alhamisi.
Ni Ijumaa siku ambayo mvu haribifu na kimbunga inaanza ifikapo saa 6 usiku.Ninadamka mapema nakuanza kuangalia televisheni napata matumani .Mafuta ya gari yanapatikana sasa ..serikali imeamua kusaidia wananchi mafuta.Hapa naona Jeuri ya Joji Kichaka...na fadhila zake .Ninafanya hima kuondoka kaskazini na kuanza upya safari.Safari sasa inaahueni...na matumani yapo .Inanichukua masaa 4 kufika katika mji wa Dallas.Imeshakuwa jioni sasa ni majira ya saa kumi..nina jinyoosha kidogo..Kuanza upya safari ya masaa 6 kuelekea kansas.
Safari inakuwa ni ndefu ila yenye matumani makubwa nimeweza kuondoka eneo la hatari.Ni saa sita usiku ninafika mji wa Kansas...ninatazama televisheni naona mvua imeshaanza kunyesha Houston na hali ya hewa ilivyotabiriwa inatoke.Ninajipatia mapumziko ya siku mbili hapa mndeni(mashambani) Kama vile wenyeji wauitavyo.
Siku ya Jumapili ninarudi nyumbani mambo yalikuwa shwari hakuna baya sana la uharibifu lililotokea.

Monday, October 03, 2005

SAFARI IMEIVA!

Siku,masaa, dakika na hata mwezi sasa unakaribia kuisha tangu ..Sekeseke za mvua za ughaibuni zijulikanazo kama hurricane zipite.Haya mambo yote yalianzia kule Luissiana ambako karibia kila mali iliteketea.,viwanda nyumba,shule ,hospital na sekta zote muhimu.
Basi shughuli na mihangaiko hayakuishia hapo basi sisi majirani wa Luissiana nasi tukapata joto ya jiwe ilikuwa ni kipindi kisicho zidi majuma manne.
Basi hizo hekaheka zikanifika hata mimi mbiu ikapigwa.. kila aliyeko eneo la hatari na hicho kimbembe basi aondeke.Na mimi nikawemo..Nayosema hapa yasikie tu yakikufika utajua.
Basi safari nikaanza siku ya Jumatano mnamo saa tano na nusu nikiwa na lengo la kuelekea Kansas mji wa mbali kutoka hapa nilipo.Muda wa makadirio wa kusafiri ikiwa masaa 6 barabarani.Haya basi hapa ndio nilijuinga na ule uhamaji mkubwa ambao unakaribia kuwekwa kwenye historia ya Marekani.
NITARUDI HIVI PUNDE KUENDELEA NA HIYO HABARI!