Pages

Tuesday, June 07, 2005

Mwanzo ni mgumu!!

Nimekuja katika lugha mama...lugha ambayo nilijifunza kuongea kabla ya hizo zingine nizijuazo leo hii.Unapojifunza kuongea huwa unajifunza kwa ishara kwanza ndipo mambo mengine yana kuja.Ndio mwanzo wa kuanzaa kusema...maaa...ukimaanisha mama..pa..ukimanisha baba..
Je ulikuwa unajua kuwa watoto wadogo ambao wanajifunza kuongea ni vizuri ukawafundisha lugha ya Ishara kwanza?Inasemekana watoto wanaojifunza lugha ya ishara wanakuwa wepesi zaidi kuongea.
Je ulikuwa unajua kuwa kujifunza chombo cha muziki humsaidia mtoto katika ufahamu wakati wa ukuaji?Hata wewe pia unaweza kujifunza...hii haijali umri wala muda...Hakuna kitu kizuri kama kufanya kile upendacho katika muda uupendao?Hakuna kitu kizuri kama kufikia lengo lako......
"HAKUNA JAMBO GUMU CHINI YA JUA"

No comments: