Pages

Wednesday, July 20, 2005

Je utaanza lini!!

Hili jambo la kujali mazingira na kuheshimu kilichoachwa na kizazi kilichopita kimekuwa ni hadithi...na simulizi sizo isha katika masikio ya wanajamii...
Utunzaji wa mazingira huanzia na wewe mwenyewe kupenda kuvuta hewa safi na kujali kizazi kinachokuja.
Ni hivi karibuni nimekuwa nikisoma makala ya mazingira na kufahamu ubaya zaidi wa hizi hewa chafu ambazo binadamu tuna tengeneza.Tunatengeneza vifaa ambavyo tunatumia kwa muda usiopungua miaka kumi huku vikiachaa maafa ya miaka mia moja ijayo.
Kila siku inapokucha mwanadamu anawaza ni jinsi gani atarahisisha hiki bila kujali ni wa ngapi atakao waathiri.Gesi za magari na mashine nzito nzito ,bandari zinazoshusha mizigo huku zikipuliza gesi zinazochafua anga na kuhatarisha maisha ya viumbe hai,watoto,watu wazima na wazee.
Ni wakati sasa umefika wa kuanza kufikiri na kuweka mtazamo makini kuhusu mazingira.Maana kizazi kijacho kitakuja kutoa hukumu ambayo wewe na mimi tungeiepuka leo hii.
Tunza mazingira,achana na tabia ya kutumia mifuko ya nailoni,chupa za plastiki,kuendesha gari kwa umbali mfupi,tumia usafiri wa umma,acha kutumia madawa kumwagilia bustanini
Kwa wale wanaoweza leo hii amua kutumia gari linalotumia maji tu ama..mafuta ya mimea.Tunza mazingira na yatakutunza..

5 comments:

Reggy's said...

Nimefurahi leo kukuta walau nimekupata kwa kiswahili, kwani kila mara nikifungua hapa naona mawenge ya kichagga. Nashauri uwe unachanganya lugha ili usituache.

Ndesanjo Macha said...

Ushauri mzuri dada yetu. Umeongelea kuhusu kuacha kutumia gari kama huendi mbali. Sio hivyo tu, kama unakwenda ofisi moja na jirani yako kuna sababu gani ya wote muende kila mtu na gari lake? leo mnaweza kutumia la huyu, kesho la yule. Wiki hii la yule, wiki ijayo la huyu. Lakini unajua tena tulivyo nani anataka kuonekana kapakia gari la mtu????

Rama Msangi said...

Aisee mtani, una akili kama tule turedio twa mbao, maana huwa tunashtuka zile nyakati za taarifa za habari basi ambazo ni nyakati muhimu sana. Nawe umeshtuka katika wakati muhimu ambao tulikuwa tunahitaji kujua mawazo yako kwa lugha rahisi bila kutafuta wakalimani, au ndio unataka kuwatafutia akina mangi ajira za ukalimani kiaina??
Tuko pamoja

Jeff Msangi said...

Mazingira ni jambo la maana sana.Nashukuru kwamba umeukumbusha umma kuhusu jambo hili.Kama ulivyosema vizazi vitatuhukumu.Tuanze sasa,hatujachelewa.Wengi wanadhani kutunza mazingira ni kutokata miti ovyo tu.Hatuwezi kuwalaumu,ndivyo wanavyofundishwa.Kuna mengi yanayochangia uharibifu wa mazingira.Umeyataja,ni vyema sote tukaanza kampeni,popote tulipo.

Ndesanjo Macha said...

Asante kwa habari hii ya digrii iliyotumwa kwa fax!
Usiwe unapotea namna hii!