Pages

Saturday, October 22, 2005

Ni kweli??

Ni imani tu au ni kweli??Hizi baadhi y aimani za watu ambozo nimekuwa nikiziskia masikioni mwangu..Na aliyenikumbusha haya ni mwana blogu mmoja aliyekuwa amepanga safari mambo yakataka kuharibika dakika za mwishohttp://jikombe.blogspot.com.
  1. Hii inatoka kule nyumbani kwangu...Rombo ...Ukiwa unasafiri usibebe ndizi za mzuzu...wala kuzila asubuhi yake safari yako itakuwa ina ..mikosi...wakimaanisha kuharibikiwa gari,kupoteza mzigo na mengi yajirijo katika safari hasa ikiwa safari ya masaa kadhaa.
  2. Si vizuri asubuhi ukakutana na mtu amevaa sweta,shati au nguo yoyote ya juu halafu amechomeka mikono ndani...kama vile watu wa vaa avyo kama unasikia baridi huku ukita kukunja mikono ndani.Chukua tahadhari na wewe fanya haraka ingiza mikono ndani uuepeku hicho kisirani.
  3. Kufagia nyumba usiku ....si vizuri
  4. Hii ni ya kimarekani...usimfagie mtu miguu...nikimaanisha ukiwa unafagia usilogwe ukamsogelea mtu na ufagio wako mbele ya miguu yake atakukimbia na kukuogopa..Hicho ni kisirani
  5. Usitumbee /kukatisha chini ya ngazi..Ngazi zile zinazotumika kuchukulia vitu juu(ladder)Hii ni hatari kabisa(Marekani)
  6. Kukaa kwenye kizingiti cha nyumba baada ya saa 12 jioni..na kama ulikuwa umelaa mchana, saa 12 jioni ikakukuta kitandani.Inasemekana unaweza kuamka unaumwa(Pwani...Tz.)

Hizi baadhi ya zile imani fulani fulani nilizozikumbuka!!

2 comments:

Jeff Msangi said...

Nadhani ni imani tu au mbinu za wazee wetu kutuweka sawa.Kwani hujawahi kusikia enzi hizo kwamba ukikojoa vichakani lazima utemee mate au sivyo titi la mama yako litavimba?

Ndesanjo Macha said...

Au ukiona zeruzeru lazima uteme mate kwenye nguo ulizovaa.