Pages

Friday, February 03, 2006

Je unajua hili??

Nipo bado ijapokuwa kuna ambao wamesema ameingia mitini huyu.Nipo katika harakati za kujifunza masuala ya kutunza afya pasipo kutumia dawa.Dawa zilizitengenezwa kwa kutumia kemikali.
Nimekuwa na furaha mno na kupenda kuwashirikisha hilli leo.Tafiti zimefanya na kugundua kuwa..
1.Kucheka ni dawa kubwa mno kwa binadamu..na kusema kuwa watoto wanauwezo wa kucheka mara 10,000 kwa juma..na watu wazima mara 5.Sasa kucheka kunasaidia kinga ya mwili kuimarika..Haya jamani hebu chekeni kidogo.
2.Tabasamu..kutabasamu kunasaidia pia kinga ya mwili..kutokana na mishipa mingi kuwa katika paji la uso ambayo huamsha sehemu zingine za mwili na kuziweka katika mwelekeo sahihi.
3.Jenga tabia ya kukumbatia watu..(hugs)Hii inasaidia mwili kukua na kujisaidiia wenyewe pasipo msaada wa kemikali.Tafiti zilibaini kuwa watoto wadogo wanaokuwa walifanyiwa majaribio.Walipewa chakula na kila kitu wanacho hitaji kwa mwili..lakini hawakukumbatiwa au kupewa busu.Wale watoto hawakukua.Sasa Jenga tabia hiyo..Jiulize leo nimekumbatia watu wangapi?Inabidi ujifunze.
4.Namalizia kwa kusema kuwa mtu wa kupenda kusema asante.Ni neno dogo lakini liseme kila wakati unapoaamka..unapokula ..Hilo neno ni zito na lina umuhimu wake na utajisikia vizuri ukilisema kwako mwenyewe na kuwaambia wengine.
Asante!

7 comments:

Ndesanjo Macha said...

Ukipata wasaa tuandikie pia kuhusu vitu kama asali, vitungee swaumu, giligilani, maji, n.k. Kucheka nalikubali ndio maana mimi hucheka mno.

Mija Shija Sayi said...

Nasikia "meditation" nayo ni nzuri kwa afya ya akili. Ukiweza na hili nalo tushushie.

Ndesanjo Macha said...

Ni sawa Mija, tafakuri/taamuli (meditation)muhimu sana kwa kutuliza akili na kupumzisha mwili. Ni njia ya kuwasiliana nawe binafsi. Tumezoea kuongea na watu wengine ila huwa hatutafuti muda wa kuingia ndani ya nafsi na akili zetu na kufanya mawasiliano nasi wenyewe. Utaona hata vitabu na simulizi mbalimbali za dini zinaelezea jinsi manabii walivyokuwa na tabia ya kuondoka mijini au kuliko na watu na kupanda milimani au kwenda msituni peke yao.

Mtafiti, ndio umeishilia cha wapi?

Vempin Media Tanzania said...

Mtafiti, tafiti zako nimezikubali je kulia nako kunasaidia nini au kuna hasara gani?

Maana kuna wengine wakilia wanapokumbuka masuala fulani fulani wanapata ahueni. Ikoje hiyo?

Maisha said...

ndesanjo,ni vitunguu swaumu bwana vitungee ndio nini?

nice blog,mtafiti...

Rundugai said...

Mtafiti tunangojea mambo mengi mzee zaidi ya kucheka,kulia na vitunguu swaumu tunakubali tupo Kijiweni tunasubiri tafiti nyingi

chemshabongo said...

umepotelea wapi mtafiti mwaka sasa unakata haupo ewani ninini kimekusibu ndugu yetu embu rudi kijiweni tuendeleze libeneke. amka!