Pages

Wednesday, April 26, 2006

motro uliaka!

Uwongo si kazikutugwa na hata mtu kuandika lakini leo nimekubali....ni muda mrefu sijawajulia hali ndugu ,jamaa, marafiki,wanafikina ,waungwana na hata maadui,Hawa wote huwa tunakutana katika haya makazi yasiyokuwa na mipaka.
Ndesanjo naona moto wa blog unawaka moto wa kasi mithili ya nyumba ya nyasi(Ngaamba fulu suti mmba sa kulya mndeni oh manya mmba sa haa uenini sejengwa kwa mfiri saba na iingua kwa dakika tanu.UUh ngaamba ngiliisha se iblogu..ngebaki nyuma foo laiki ikoti...
karibuni wooose fuu mmba!

Friday, February 03, 2006

Je unajua hili??

Nipo bado ijapokuwa kuna ambao wamesema ameingia mitini huyu.Nipo katika harakati za kujifunza masuala ya kutunza afya pasipo kutumia dawa.Dawa zilizitengenezwa kwa kutumia kemikali.
Nimekuwa na furaha mno na kupenda kuwashirikisha hilli leo.Tafiti zimefanya na kugundua kuwa..
1.Kucheka ni dawa kubwa mno kwa binadamu..na kusema kuwa watoto wanauwezo wa kucheka mara 10,000 kwa juma..na watu wazima mara 5.Sasa kucheka kunasaidia kinga ya mwili kuimarika..Haya jamani hebu chekeni kidogo.
2.Tabasamu..kutabasamu kunasaidia pia kinga ya mwili..kutokana na mishipa mingi kuwa katika paji la uso ambayo huamsha sehemu zingine za mwili na kuziweka katika mwelekeo sahihi.
3.Jenga tabia ya kukumbatia watu..(hugs)Hii inasaidia mwili kukua na kujisaidiia wenyewe pasipo msaada wa kemikali.Tafiti zilibaini kuwa watoto wadogo wanaokuwa walifanyiwa majaribio.Walipewa chakula na kila kitu wanacho hitaji kwa mwili..lakini hawakukumbatiwa au kupewa busu.Wale watoto hawakukua.Sasa Jenga tabia hiyo..Jiulize leo nimekumbatia watu wangapi?Inabidi ujifunze.
4.Namalizia kwa kusema kuwa mtu wa kupenda kusema asante.Ni neno dogo lakini liseme kila wakati unapoaamka..unapokula ..Hilo neno ni zito na lina umuhimu wake na utajisikia vizuri ukilisema kwako mwenyewe na kuwaambia wengine.
Asante!

Friday, January 06, 2006

Heri ya mwaka mpya.

Nglaafo ngera ya sisi,ngilemaa mwaka..Heri ya mwaka huu uhiyaa kwa moni wasomii wakwa.
Nimerudi mwaka mpya hivi nikiwa na mambo mengi ..sitaki kutumia usemi aliotumia mgombea uraisi wa wadanganyika..nitake kuwakoga na nyie wengine.Haya Basi mwaka umeanza na vijimambo vyake..
Nipende tu kuwashirikisha wanaglobu wenzangu huu mwaka nimepania na ninaweka mtazamo makini nataka kusoma vitabu.Macha alishanieleza ni kwa kiasi gani ukisoma unapata mwanga..sasa mimi mwenzenu nia yangu kubwa ni kuhangaika na vitabu.
Hebu jiulize ni vitabu gani hivi huyu mtafiti anataka kusoma??????
Nimeanza kusoma vitabu vya tiba za asili,tiba za matunda,majani ,maji,mizizi iliradi kisiwe kinahusisha mashine na kuongezwa kemikali.Hiyo ndio hoja nayoanza nayo mwaka huu.Kwa hiyo kaaeni mkao wa kula,angalau kila siku naweza kuwatumia dawa kidogo mkasoma na kutumia.
Nilishawadokeza ya mkojo kidogo,sasa nitaileta kwa undani..na kwa taarifa yenu kama kuna mtu anata kujaribu nasema fanya utaaona matokeo yake.Hapa leo sipo kutoa shuhuda lakini nasema mwaka huu najali afya yangu na wanablog wenzangu nasema afya yako ni muhimu.
Haya kwa taarifa ya juu juu..anza kula vitu ambavyo unaweza KUTAAMKA KWA ULIMI WAKO ,UKALA.Hicho unaweza kutumia..kama huwezi basi ujue si kizuri kwa afya yako.
Mwaka mpya huu jamani mlio na watoto muache kuwalishe zile wnazoita fomula..maana ni mengi yaliyopo huko,watumiaji wa manukato hasa ya kwenye makwapa(Deodorants)Muache hasa wanawake inasemekana inachangia kwa kiasi kikubwa saratani ya ziwa.Mpo hapo?Watumiaji wa majiko ya kupasha moto chakula(microwave) macho haya tunayapoteza.
Uhondo wa ngoma uingie ucheze na shughuli ipate mkunga!