Pages

Friday, December 23, 2005

NINGEKUWA NA MABAWA....

Ningekuwa na mabawa ningeruka upesii..Nyumbani mbali..ni nani asiyepata ugonjwa wa kukumbuka nyumbani hasa inapofika wakati wa sikukuu???????Ninatembea barabarani,ninatazama huku na kule nikijaribu kubadili mazingira kwa akili na macho yangu,nafunga macho, nafungua ni pale pale ambapo nimekuwepo,hakuna jipya zaidi ya mapambo na harakati za sikuuu..
Heka heka za manunuzi ya mwisho mwisho wa sikukuuu ya Noeli ndio hivyo yanatia tamati muda si mrefu.Ni maduka makubwa machache ambayo yatakuwa wazi.Watu wanasafiri,barabara ,viwanja vya ndege vimejaa watu wako mbioni kuungana na familia na mrafiki kwa ajili ya sikuuu.Hizi ni harakati ambazo zinaendelea kwa hali ya juu hapa nilipo.Wafanyao kazi,wengi wao wanasiku kadhaa za mapumziko.Ni shamra shamra zinaendelea hapa Nyumbani kwa Joji Kichaka.
Ninakumbuka nyumbani,ninakumbuka Tanzania,ninakumbuka Dar-es salaam,Ninakumbuka Rombo.Nauli za kuelekea Kilimanjaro zimekuwa "iyo la njofuu"Kila mtu anataka kupanda basi la Meridia kwenda Rombo.Watu wamekuwa wengi nauli haishikii..lakini hakuna anayekubali kusherehekea noeli darisalama.Maamuzi ya kukaa kwenye kigoda masaa nane yanawakumba wasafiri wa dakika za mwisho .Hiyo ndio hali halisi,kituo cha basi cha ubungo kimeshehena watu..ni majira ya saa tisa na nusu na kumi alfajiri mabasi yanaondoka.Yameanza kuwasha taa na honi zikipigwa kwa wingi.Ni mashamu shamu na manjonjo ya sikukuu tu hayo.Bila kusahau polisi wa usalama barabarani nao wanamengi ya kusema na madereva.
Ni foo shuruni kulwayaa mndeni,waiinu waliisha isherikia krismasi,mengele si meshiha,si isafii,umbe sa amii fo shii,mahorima.Kwentrwe maruwa,umbe silishinjwa,mburu,kisusio,umbeke kwentre kila mrii..ndisi na mshele umewa tayari kwa jumapili we kora pilau na shapati.Kwa fungua redioo waishua foo Kenya wakakaba Jim revees nyimbo saChirsmas.Foo makaniseni kwentrewe misa sa kiyoo,hashe hashe kona waliimba.Ngaamba kwentre chrismas mndeni laaya handu we manya kwetre skukuu.
HASHE HASHE KONA !!

3 comments:

Ndesanjo Macha said...

Justin Kalikawe alikuwa na wimbo mmoja akisema, "Ningekuwa na mabawa ningeruka kama ndege, lakini mimi ni mwanadamu ninayetembea ardhini."

Mija Shija Sayi said...

Mtafiti, mwenzio bado naisubiri habari nzima ya mkojo na matumizi yake.

Mwaka mpya mwema.

mloyi said...

Ungukewa na mabawa
ungeruka kama ndege
nasi tungekuona juu angani
karibuyo tusingejongea
mafua ya ndege twayasikia.