Hivi siwezi kuaminini mwezi sasa umepita tangu niingie humu ndani ya nyumba yangu kusema lolote.Hivi ni mwaka huu umekuwa mfupi au nimekuwa na mambo mengi kIasi nasema kuwa muda ulikuwa mdogo.
kuna mwanablogu mmoja huwa anasema masaa 24 huwa haya mtoshi na sema tena sasa nimeamini nitaacha kutania ambao wanadai masaa 36.
Mchana wa leo umekuwa mtulivu kidogo kwangu baada ya kumaliza mitihani yangu ya muhula kama lisaa limoja lililopita.Nimerudi katika ulimwengu wa kutoa maoni yangu kwa kutumia mtandao.
Ulimwengu wa Blogu umekuwa na mafanikio bila kipingamizi na kuna mwamko wa pekee unaendelea katika jamii ya waafrika wazungumzao kiswahili.Na hao sio wengine ni wa Tanzania wenzangu ambao wamekuwa wakijiunga kila siku kukicha katika hii tekinolojia.Nasema tena karibuni watanzania wenzangu tuweke yanayotusibi hata kama hawasomi watayasikia kupita hapa ama pale.Hongera sana kwa wale ambao wamekuwa wakijiunga kwa wingi,naweza kusema mwaka 2005 umekuwa na changamoto ya pekee kwa wana globu.Hongera kwa watu ambao hawako nyuma kutupa viunganishi vya globu mpya mara zinapoingia..si Mwingine bali ni NDESANJO.http://jikombe.blogspot.com
3 comments:
Umesema sawa, "hata kama hawatasoma watayasikia hapa au pale." Wasiposoma watayasikia kwa waliosoma au kwa waliosikia toka kwa walisoma au kwa waliosikia toka kwa waliosikia kwa wale waliosoma.
Nawe kwa kuingiaga mitini! Heri umerudi.
Kumekucha kwelikweli! Blogu zinawasha moto wa amani na mijadala ya vina, sio kama makampu ambako ni maficho ya vibaka.
Tumeweza kuungana na kufahamiana, matusi sijasikia mazuri sana haya naomba mwaka 2006 yaendelee. Ndesanjo alituelekeza wengi hapa, akatupa vibaraza vya kukaribishia wageni, Mtafiti siku mtu akijitambulisha kwako, mimi ninaitwa mloyi, atashangaa sana? Hiyo ni kazi ya blogu.
Tujifunze zaidi hapa.
MAKOFI KWA KAKA NDESANJO! japo mie blogu langu limechamsha kwa ustaarabu na bado ni mgonjwa kwa kutumia viunganishi, lakini naamini mungu atanipa muda wa kujifunza jinsi ya kuvitumia. nitasoma tena maagizo ya kaka ndesanjo na kujifunza kutengeneza na kupamba blogu lifannane fanae na haya ya kwenu!
amini usiamini bwana mtafiti, hii mibwabwajo yetu kwa kiasi kikubwa imeongeza uelewa wa jamii kwa kiasi kikukwa achilia mbali kuvunja ile kanuni ya kuendesha cults - (mtanisaidia kiswahili sanifu hapa). katika cults - mfano ya kibwetere mawasilano kati ya wanajumuiya ya cults hukatazwa. mawasiliano yanayoruhusiwa ni kati ya mwanajumuiya na mkuu wa hekalu. hivyo ndivyo wana jumuiya ya cult ya kibwetere walivyoteketea!
Tanzania ilikuwa cult ya nyerere kwa muda mrefu. sasa utagundua kitu kinachofanyika hapa sasa ndio kimewapa nguvu hata waheshimiwa wagunge kuung'oa mbuyu juzi bungeni!
amini usiamini, hata sehemu kubwa wa maswali waliyokumbana nayo wahishimiwa wakati wa kampeni yalitokea humu humu!
aluta continua!
Post a Comment