Pages

Monday, November 14, 2005

Sema utakacho.

Mfiri n'ganyaa fo nyumaa nilikuwa natembelea blogu mbali mbali na kuangalia nini hasa kinaongelewa na nini hasa, nani anajisikia kuandika nini.
Nilifurahi sana na dhani nilitumia muda wa masaa mawili tu kusoma nini wanablogu kama mimi wanasema na kujifunza.
Siku kadhaa niliahidi nitaandika kuhusu televisheni.Laah leo nimepata zuri zaidi lipi hilo.
Nimeingia katika fani ya afya.Nilikuwa nasoma kuhusu mkojo na tiba zake.Ahh ni mengi nitaandika tena .Bado nasoma makala tofauti tofauti kupitia wandishi tofauti na kurasa tofauti za mtandao.

Monday, November 07, 2005

je huu ni ubaguzi??

Nina kazi ya darasani ya kuandika kuhusu jamii na utazamaji wa luninga.nimeshindwa kusema ama kuandika vizuri kutumia kiswahili hata kile kichaga.mada yenyewe inasema hivi"Ethinicity&race has been a long time issue on television."
Hapa nitakuwa nazungumziua jinsi televisheni zimekuwa zikionjesha aina fulani za jamii na yanayowazunguka.. katika vipindi vya luninga kama "friends"Bill Cosby"oprah na wengineo.Je wanaonyesha ule uhalisia wa jamii zao.?Je jamii ndogo kama za wamarekani halisi (wahindi wekundu)wamarekani wa kiasia?Je hawa wamekuwa waki wakilishwa katika hivi vipindi?Nitarejea nikimaliza kuandika kazi yangu ya shule.Hii mada imenikumbusha mengi.