Safari ikaanza kuelekea huko ambako kimbunga kilikisiwa kutokufika.Safari ilianza kwa matumani huku kila mtu akiwa na matumaini ya kufika salama.Kasheshe na mauza uza uza yote yalikuwa barabarani.Ulikuwa ni msongamano wa magari ambao ulikuwa wa kwanza kwa mimi kuona kwa macho yangu.Na huu msongamano ulikuwa katika zile barabara za juu ambazo hutumika kwa mwendo kasi.magari hayasogei...hali ya hewa inazidi kuwa ya hatari.Huku kwenye redioni, meya wa jiji anazidi kuonya kuhusu umuhimu wa kuhama mji na maeneo ya hatari.
Nimekesha usiku kucha barabarani...hakuna matumaini yoyote yale sasa ni saa 12 asubuhi..sijaweza hata kutoka nje ya mji.Muda wa saa 24 nipo barabarani sijaweza hata kufika upande wa kaskazini wa mji ninaoishi.Imefika saa 1 asubuhi nasikiliza redio tunaelezwa kwamba barabara ya kuelekea kusini itafungwa iruhusu magari kuelekea kaskazini.Nimechoka nina usingizi ninahofu ya mvua kuanza nikiwa barabarani.Ninahofu ya kupoteza maisha ,majira ya joto hayaisha rasmi katika huu mji wa Houston joto ni kali mno, la nyuzi za farenihaiti 94.
Nimechoka sasa naona hakuna matumani ...ninafikiri jambo moja tu hapa nilipo nikaribu na nyumbani kwa rafiki yangu aishiye kaskazini.Ninakata shauri na kwenda kupumzika kwake...huu ni mchana wa siku ya alhamisi alasiri.Hali ya hewa bado ni mbaya upepo unaoleta hilo janga unazidi kuvuma.Mawasiliano ya simu yameshakuwa mabaya kutokana na kila mtu kuwa ni mtumiaji wa simu kwa wakati mmoja.Mafuta ya magari sasa yamekwisha katika vituo matumaini ya safari yanapungua.Ninakaza roho nina pumzisha mwili usiku wa alhamisi.
Ni Ijumaa siku ambayo mvu haribifu na kimbunga inaanza ifikapo saa 6 usiku.Ninadamka mapema nakuanza kuangalia televisheni napata matumani .Mafuta ya gari yanapatikana sasa ..serikali imeamua kusaidia wananchi mafuta.Hapa naona Jeuri ya Joji Kichaka...na fadhila zake .Ninafanya hima kuondoka kaskazini na kuanza upya safari.Safari sasa inaahueni...na matumani yapo .Inanichukua masaa 4 kufika katika mji wa Dallas.Imeshakuwa jioni sasa ni majira ya saa kumi..nina jinyoosha kidogo..Kuanza upya safari ya masaa 6 kuelekea kansas.
Safari inakuwa ni ndefu ila yenye matumani makubwa nimeweza kuondoka eneo la hatari.Ni saa sita usiku ninafika mji wa Kansas...ninatazama televisheni naona mvua imeshaanza kunyesha Houston na hali ya hewa ilivyotabiriwa inatoke.Ninajipatia mapumziko ya siku mbili hapa mndeni(mashambani) Kama vile wenyeji wauitavyo.
Siku ya Jumapili ninarudi nyumbani mambo yalikuwa shwari hakuna baya sana la uharibifu lililotokea.