Pages

Monday, September 12, 2005

Yasikilizie kwenye bomba!!

Haya jamani kwa wana blog ambao walikuwa wanashangaa huyu mtu kapotelea wapi...???Basi ondoeni wasiwasi nilikumbwa na matatizo ya Rita..
Nasema tena haya mambo ya mvua za ughaibuni na upepo na vimbunga hivyo..Niliviona huku niliko.Almanusura maji yazidi unga .
Nina mengi ya kusema na kuandika ...Ndio kwanza huku mambo yamerudi kwenye mstari rasmi leo.

Thursday, September 08, 2005

Nimekubali

Hayawi hayawi sasa mambo yanazidi kuwa matamu katika ulimwengu wa kublog wa watanzani.
Yule mpiga picha maarufu na machachari wa Tanzania yupo ndani ya nyumba mtembelee tafadhali.www.michuzi.blogspot.com

Wednesday, September 07, 2005

Mnyonge Mnyongeni!!!

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni...unaweza ukakaa ukaona yanayotendeka hapa ulimwenguni ni kama ndoto za Alinacha kumbe ni kweli.
Ni juma hili ulimwengu umeshuhudi watu wakifa kwa mafuriko ya maji,njaa,kukosa msaada katika nchi ambayo inaheshimika duniani kwa ubabe.Na ni ubabe hasa wa kisiasa kiuchumi,kivita ikiacha watu wake wakigharaghara barabarani.Ni nchi hii hii ambayo inaendeleza ubabe kule mashariki ya mbali ikidai inawasaidia .Laa huku wakiwa na mambo na mipango yao mingi nyuma ya pazia.
Hali ya maisha ya hawa ndugu zetu,jamaa wa luisiana inasikitisha...Ilichukua serikali kufahamu ,maaafa ni makubwa baada ya juma.Mbona wao wanakuwa wababe hasa kwa watu wa nje kuliko kwa ndugu zao wa ndani.hapa mimi najiuliza au tunarudi kulekule kwamba Maskini ni maskini??Hata hivyo jamani kuokolewa siku za mwanzo haikuwa haki yake???Si hawa watu ambao wanapiga vita vifo visivyokuwa na misingi???Au tunarudi pale kwenye suala la rangi?
Nimekumbuka iliwachuikua muda kufikiri hilo kwa sababu ya wengi waliokuwa kule walikuwa ni weusi..na viongozi walio juu ni weupe.hivyo swala la kufikiria mtu mweusi lilikuwa mbali kiidogo.Inasikitisha kuona jinsi watoto wanavyopata shida wazee,wasiojiweza.
Ama hakika sasa Dunia imeona upande wa pili wa sarafu..Iliku ikishuhudia picha za watoto wa Sudani na nchi nyingine za kiafrika zikitaabika..Sasa wameona hata Marekani inaweza kuwaacha wananchi wake nao waonekane kwenye CNN .

Friday, September 02, 2005

petrilori

linu ngimemannya uishwa wa fitrwa fya Iraq..Mafutra yameituma ho dokaa yalishika dola itanu ha Marikani.Ngaammba Kishaka alefikiri iinda Arabuni mafutra yangesokaa yave sumni,laa mmeku yameinda hoo dokaa.Na mfua sa Lusiana.
Amba matukiooa yaika soni,mafutra,mfua,wanajeshi waliifa bure kulya irak.
Ngaamba pertilori ishingi nga foo Tz???