Pages

Friday, February 03, 2006

Je unajua hili??

Nipo bado ijapokuwa kuna ambao wamesema ameingia mitini huyu.Nipo katika harakati za kujifunza masuala ya kutunza afya pasipo kutumia dawa.Dawa zilizitengenezwa kwa kutumia kemikali.
Nimekuwa na furaha mno na kupenda kuwashirikisha hilli leo.Tafiti zimefanya na kugundua kuwa..
1.Kucheka ni dawa kubwa mno kwa binadamu..na kusema kuwa watoto wanauwezo wa kucheka mara 10,000 kwa juma..na watu wazima mara 5.Sasa kucheka kunasaidia kinga ya mwili kuimarika..Haya jamani hebu chekeni kidogo.
2.Tabasamu..kutabasamu kunasaidia pia kinga ya mwili..kutokana na mishipa mingi kuwa katika paji la uso ambayo huamsha sehemu zingine za mwili na kuziweka katika mwelekeo sahihi.
3.Jenga tabia ya kukumbatia watu..(hugs)Hii inasaidia mwili kukua na kujisaidiia wenyewe pasipo msaada wa kemikali.Tafiti zilibaini kuwa watoto wadogo wanaokuwa walifanyiwa majaribio.Walipewa chakula na kila kitu wanacho hitaji kwa mwili..lakini hawakukumbatiwa au kupewa busu.Wale watoto hawakukua.Sasa Jenga tabia hiyo..Jiulize leo nimekumbatia watu wangapi?Inabidi ujifunze.
4.Namalizia kwa kusema kuwa mtu wa kupenda kusema asante.Ni neno dogo lakini liseme kila wakati unapoaamka..unapokula ..Hilo neno ni zito na lina umuhimu wake na utajisikia vizuri ukilisema kwako mwenyewe na kuwaambia wengine.
Asante!