Pages

Friday, December 23, 2005

NINGEKUWA NA MABAWA....

Ningekuwa na mabawa ningeruka upesii..Nyumbani mbali..ni nani asiyepata ugonjwa wa kukumbuka nyumbani hasa inapofika wakati wa sikukuu???????Ninatembea barabarani,ninatazama huku na kule nikijaribu kubadili mazingira kwa akili na macho yangu,nafunga macho, nafungua ni pale pale ambapo nimekuwepo,hakuna jipya zaidi ya mapambo na harakati za sikuuu..
Heka heka za manunuzi ya mwisho mwisho wa sikukuuu ya Noeli ndio hivyo yanatia tamati muda si mrefu.Ni maduka makubwa machache ambayo yatakuwa wazi.Watu wanasafiri,barabara ,viwanja vya ndege vimejaa watu wako mbioni kuungana na familia na mrafiki kwa ajili ya sikuuu.Hizi ni harakati ambazo zinaendelea kwa hali ya juu hapa nilipo.Wafanyao kazi,wengi wao wanasiku kadhaa za mapumziko.Ni shamra shamra zinaendelea hapa Nyumbani kwa Joji Kichaka.
Ninakumbuka nyumbani,ninakumbuka Tanzania,ninakumbuka Dar-es salaam,Ninakumbuka Rombo.Nauli za kuelekea Kilimanjaro zimekuwa "iyo la njofuu"Kila mtu anataka kupanda basi la Meridia kwenda Rombo.Watu wamekuwa wengi nauli haishikii..lakini hakuna anayekubali kusherehekea noeli darisalama.Maamuzi ya kukaa kwenye kigoda masaa nane yanawakumba wasafiri wa dakika za mwisho .Hiyo ndio hali halisi,kituo cha basi cha ubungo kimeshehena watu..ni majira ya saa tisa na nusu na kumi alfajiri mabasi yanaondoka.Yameanza kuwasha taa na honi zikipigwa kwa wingi.Ni mashamu shamu na manjonjo ya sikukuu tu hayo.Bila kusahau polisi wa usalama barabarani nao wanamengi ya kusema na madereva.
Ni foo shuruni kulwayaa mndeni,waiinu waliisha isherikia krismasi,mengele si meshiha,si isafii,umbe sa amii fo shii,mahorima.Kwentrwe maruwa,umbe silishinjwa,mburu,kisusio,umbeke kwentre kila mrii..ndisi na mshele umewa tayari kwa jumapili we kora pilau na shapati.Kwa fungua redioo waishua foo Kenya wakakaba Jim revees nyimbo saChirsmas.Foo makaniseni kwentrewe misa sa kiyoo,hashe hashe kona waliimba.Ngaamba kwentre chrismas mndeni laaya handu we manya kwetre skukuu.
HASHE HASHE KONA !!

Wednesday, December 14, 2005

Kumekucha.

Hivi siwezi kuaminini mwezi sasa umepita tangu niingie humu ndani ya nyumba yangu kusema lolote.Hivi ni mwaka huu umekuwa mfupi au nimekuwa na mambo mengi kIasi nasema kuwa muda ulikuwa mdogo.
kuna mwanablogu mmoja huwa anasema masaa 24 huwa haya mtoshi na sema tena sasa nimeamini nitaacha kutania ambao wanadai masaa 36.
Mchana wa leo umekuwa mtulivu kidogo kwangu baada ya kumaliza mitihani yangu ya muhula kama lisaa limoja lililopita.Nimerudi katika ulimwengu wa kutoa maoni yangu kwa kutumia mtandao.
Ulimwengu wa Blogu umekuwa na mafanikio bila kipingamizi na kuna mwamko wa pekee unaendelea katika jamii ya waafrika wazungumzao kiswahili.Na hao sio wengine ni wa Tanzania wenzangu ambao wamekuwa wakijiunga kila siku kukicha katika hii tekinolojia.Nasema tena karibuni watanzania wenzangu tuweke yanayotusibi hata kama hawasomi watayasikia kupita hapa ama pale.Hongera sana kwa wale ambao wamekuwa wakijiunga kwa wingi,naweza kusema mwaka 2005 umekuwa na changamoto ya pekee kwa wana globu.Hongera kwa watu ambao hawako nyuma kutupa viunganishi vya globu mpya mara zinapoingia..si Mwingine bali ni NDESANJO.http://jikombe.blogspot.com