Pages

Friday, January 06, 2006

Heri ya mwaka mpya.

Nglaafo ngera ya sisi,ngilemaa mwaka..Heri ya mwaka huu uhiyaa kwa moni wasomii wakwa.
Nimerudi mwaka mpya hivi nikiwa na mambo mengi ..sitaki kutumia usemi aliotumia mgombea uraisi wa wadanganyika..nitake kuwakoga na nyie wengine.Haya Basi mwaka umeanza na vijimambo vyake..
Nipende tu kuwashirikisha wanaglobu wenzangu huu mwaka nimepania na ninaweka mtazamo makini nataka kusoma vitabu.Macha alishanieleza ni kwa kiasi gani ukisoma unapata mwanga..sasa mimi mwenzenu nia yangu kubwa ni kuhangaika na vitabu.
Hebu jiulize ni vitabu gani hivi huyu mtafiti anataka kusoma??????
Nimeanza kusoma vitabu vya tiba za asili,tiba za matunda,majani ,maji,mizizi iliradi kisiwe kinahusisha mashine na kuongezwa kemikali.Hiyo ndio hoja nayoanza nayo mwaka huu.Kwa hiyo kaaeni mkao wa kula,angalau kila siku naweza kuwatumia dawa kidogo mkasoma na kutumia.
Nilishawadokeza ya mkojo kidogo,sasa nitaileta kwa undani..na kwa taarifa yenu kama kuna mtu anata kujaribu nasema fanya utaaona matokeo yake.Hapa leo sipo kutoa shuhuda lakini nasema mwaka huu najali afya yangu na wanablog wenzangu nasema afya yako ni muhimu.
Haya kwa taarifa ya juu juu..anza kula vitu ambavyo unaweza KUTAAMKA KWA ULIMI WAKO ,UKALA.Hicho unaweza kutumia..kama huwezi basi ujue si kizuri kwa afya yako.
Mwaka mpya huu jamani mlio na watoto muache kuwalishe zile wnazoita fomula..maana ni mengi yaliyopo huko,watumiaji wa manukato hasa ya kwenye makwapa(Deodorants)Muache hasa wanawake inasemekana inachangia kwa kiasi kikubwa saratani ya ziwa.Mpo hapo?Watumiaji wa majiko ya kupasha moto chakula(microwave) macho haya tunayapoteza.
Uhondo wa ngoma uingie ucheze na shughuli ipate mkunga!